Wito wa Kwanza wa Ufadhili wa Mapendekezo wa 2022

Mfuko wa Kimataifa kwa Vyombo vya Habari vyenye Maslahi ya Umma (IFPIM) ni mpango mpya, imara wa kimataifa ulioundwa ili kusaidia vyombo vya habari vinavyojitegemea vyenye maslahi ya umma hasa katika mazingira ya mapato ya chini na ya kati na kuunga mkono masuluhisho ya muda mrefu ya hali za sasa zinazozuia vyombo vya habari vinavyojitegemea kujifadhili.

Mfuko unalenga kuongeza sana kiwango cha nyenzo zinazopatikana ili kuunga mkono uandishi wa habari unaoaminika, wenye maadili na ukweli, na kuwezesha vyombo vya habari kufanya kazi kwa ajili ya demokrasia. Maelezo zaidi kuhusu Mfuko yanaweza kupatikana kwenye ifpim.org.

Maendeleo makubwa yamepatikana na mfuko huu, na ukiwa bado katika hatua za awali za kuanzishwa, umepata ufadhili wa kutosha wa kuzindua wito mdogo wa awali wa mapendekezo. Wito huu wa mapendekezo ni wa kwanza kati ya mfululizo wa fursa za ufadhili.

Kisanduku cha 1 : Ufafanuzi wa Vyombo vya Habari vyenye Maslahi ya Umma

IFPIM inafafanua Vyombo vya Habari vyenye Maslahi ya Umma kama vyombo vya habari:

 • ambavyo havidhibitiwi na vinavyojitegemea;
 • vinavyolenga kufahamisha umma kuhusu maswala yanayohusu maisha yao kwa njia zinazozingatia maslahi ya umma badala ya masilahi yoyote ya kisiasa, kibiashara au kikundi;
 • ambavyo huwezesha mijadala ya umma na mazungumzo katika jamii; na
 • vinavyowawajibisha watu walio madarakani kwa niaba ya maslahi ya umma.

Inamaanisha midia yenye maadili na ya kuaminika inayofanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu wote katika jamii yote, sio tu watu walio na uwezo au pesa za kulipia au kushawishi vyombo vya habari. Vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma vinaweza kuwa vya kibiashara, vya utumishi kwa umma au vyombo vya habari vya jamii na kusambazwa mtandaoni, kutangazwa, kupitia magazeti au chaneli nyinginezo.

"Bila upatikanaji wa habari binafsi za kuaminika, watu wengi huachwa gizani, serikali zinakuza ufisadi na taasisi za kidemokrasia zinakuwa bandia."

Mark Thompson na Maria Ressa

Wenyeviti Wenza, IFPIM

Lengo la ufadhili huu

Wito huu wa kwanza wa ufadhili umeundwa kama sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuendeleza na kujenga upya vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma wakati wa shinikizo kubwa la kiuchumi kwa nia ya kuhakikisha kwamba tunaendelea kuunga mkono uandishi wa habari unaozingatia maslahi ya umma na kuongeza watazamaji na wasilikilizaji na mahusiano.

Katika wito huu wa kwanza, maombi ya ufadhili yanapaswa kuhusisha moja au zaidi ya malengo yafuatayo:

 • kuendelea kutoa na kusambaza taarifa za vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma ili kuendeleza jukumu na athari zake katika jamii katika muktadha wa hali mbaya ya soko na mahitaji muhimu ya ufadhili.
 • uundaji wa mbinu za kutaka makuu za kushughulikia changamoto za upotoshaji katika jamii, ikiwa ni pamija na kujaribu aina mpya za kuwahusisha watazamaji na wasikilizaji na kwa kushirikiana na wahusika wengine katika mfumo wa ikolojia wa midia au asasi za kiraia.
 • Kuongeza na kuwahusisha watazamaji na wasikilizaji, ikiwa ni pamoja na watu wanaotaka kushughulikia mahitaji ya hadhira isiyohudumiwa ipasavyo
 • kuboresha uwakilishi wa jamii katika mfumo wa ikolojia wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kukuza utofauti katika chumba cha habari na kutangaza masuala na jumuiya ambazo hazijaripotiwa sana

Upeo wa kijiografia

Katika wito huu wa kwanza, mihutasari ya mradi inaalikwa kutoka kwa mashirika ya habari yenye rekodi thabiti ya uandishi wa habari unaozingatia maslahi ya umma katika nchi zilizoorodheshwa hapa chini.

 • Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara: Ghana, Kenya, Niger, Senegal, Sierra-Leone, Afrika Kusini;
 • Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini: Lebanon, Tunisia;
 • Caribbean, Amerika ya Kati na Kusini: Brazil, Colombia, Mexico;
 • Asia na Pasifiki: Afghanistan, Malaysia, Nepal, Philippines;
 • Ulaya Mashariki : Georgia, Ukraine.

Lazima ruzuku zisaidie vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma katika mojawapo ya nchi zilizoorodheshwa hapo juu. Wito wa siku zijazo utajumuisha nchi nyingi zaidi kuliko zilizoorodheshwa hapa.

Kiasi cha ruzuku na ustahiki

Kiasi cha ruzuku: Ruzuku zitatolewa kwa muda wa hadi miaka 2. Tunatarajia ruzuku nyingi kuwa kati ya $80,000 hadi $350,000. IFPIM inazingatia hitaji la kusawazisha hitaji la ufadhili muhimu na hatari zinazohusiana na kutegemea sana mfadhili mmoja. Kiasi cha ruzuku kwa mwaka kwa ujumla kinatarajiwa kuwa kati ya 10% – 30% ya bajeti ya kila mwaka ya shirika.

Aina ya mwombaji: Ruzuku zinatolewa kwa mashirika ya habari pekee na hazipeanwi kwa watu binafsi au wahusika wengine walio katika mfumo wa ikolojia wa vyombo vya habari kwa wito huu wa ufadhili. Mashirika ya habari yanafafanuliwa kama mashirika yaliyo na shirika la kisheria lililosajiliwa linalohusika katika kutoa na kusambaza habari kwa umma kupitia njia ya mawasiliano ya umma.  Mashirika ya habari ya faida na yasiyo ya faida yanaweza kutuma maombi ya ufadhili. Lazima waombaji wawe na mapato ya sasa ya angalau $50,000 kwa mwaka ili watume maombi. Tunatarajia waombaji wengi wawe na mapato yanayozidi $50,000 kwa mwaka.

Waombaji watahitaji kuonyesha kwamba kwa kweli hao ni vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma kama ilivyofafanuliwa katika Kisanduku cha 1. Wakiendelea kufanya hivyo, tutazingatia maombi kutoka kwa mashirika ya habari katika: aina zote za majukwaa (ya mtandaoni na nje ya mtandao); watazamaji na wasikilizaji wote (kutoka vyombo vya habari vya kitaifa hadi vya eneo husika na vya jamii); nafasi zote za uhariri (waandishi wa habari wa mada za jumla na mada maalum zaidi); na kiwango cha ukomavu wa shirika (vyombo vya habari vilivyoanzishwa kitambo na midia mpya zaidi).

Mchakato wa Kutuma Maombi na Uteuzi

Mashirika yanayotaka kutuma maombi ya ufadhili katika wito huu wa kwanza, kwa mara ya kwanza, yatahitaji kuwasilisha muhtasari mfupi wa mradi (takriban kurasa 3 hadi 4) unaofafanua:

 • shirika la mwombaji, pamoja na ikiwa inazingatia ufafanuzi wa IFPIM wa vyombo vya habari vyenye maslahi ya umma; na
 • jambo ambalo mwombaji anatarajia kutimiza kwa ufadhili wa IFPIM.

Fomu za muhtasari wa mradi zinaweza kupatikana kwa kufuata kiungo hiki.

Maelezo ya ziada na mwongozo unapatikana kupitia viungo vilivyo hapa chini, ambavyo vinajumuisha ‘maswali yanayoulizwa mara kwa mara’. Ikiwa swali lako halijajibiwa tafadhali tuma swali lako kabla ya tarehe 20 Mei kwenye: opencall@ifpim.org na uandike mada ya barua pepe yako ‘Swali linalohusiana na Wito wa Ufadhili wa 1’. Tafadhali jua kwamba hatutajibu barua pepe mahususi lakini tutasasisha ‘maswali yanayoulizwa mara kwa mara’ wakati wa mchakato wa kutuma maombi.

Mihutasari ya mradi itazingatiwa na kuorodheshwa ili izingatiwe zaidi. Waombaji waliochaguliwa wataalikwa ili watoe pendekezo la kina zaidi, ikiwa ni pamoja na maelezo zaidi kuhusu fedha, athari inayotarajiwa na hati kwa ajili ya uchunguzi mahususi wa shirika husika. Maamuzi ya mwisho ya ufadhili yatafanywa kulingana na vigezo vya uteuzi. Tunatarajia kupata idadi kubwa ya waombaji, ambapo ni wachache tu ndio watakaofaulu.

Rekodi ya matukio

Jumatatu 13 Juni 2022

Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha muhtasari wa mradi (hadi saa 11:59 usiku GMT). Waombaji watapokea barua pepe inayothibitisha kuwa tumepokea ombi lako.

Jumatatu 11 Julai 2022

Waombaji wote wamejulishwa kuhusu matokeo ya mchakato wa kuchagua watu. Waombaji waliochaguliwa watahitajika kuwasilisha pendekezo la kina zaidi. Mwongozo zaidi utatolewa kwa waombaji waliochaguliwa katika hatua hii.

Jumatatu 15 Agosti 2022

Tarehe ya mwisho ya waombaji waliochaguliwa kuwasilisha mapendekezo (hadi saa 11:59 usiku GMT).

Alhamisi 15 Septema 2022 kuendelea

Uteuzi wa seti ya awali ya wanaruzuku ifikapo tarehe 15 Septemba, na uteuzi wa wafadhili wa ziada ifikapo tarehe 15 Novemba. Waombaji ambao wamekataliwa wakati wa mchakato wa uteuzi watajulishwa kuhusu matokeo muda mfupi baada ya uamuzi kufanywa. Waombaji waliochaguliwa wataendelea katika awamu ya kufanya mkataba. Utoaji wa fedha utafanyika muda mfupi baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya ruzuku lakini ratiba sahihi itategemea mamlaka.

Vigezo vya kustahiki na uchaguzi

Hatua ya kwanza ya mchakato wetu wa uchaguzi inategemea ukaguzi wetu wa muhtasari wa mradi wa waombaji, taarifa ya shirika na historia na itazingatia vigezo vifuatavyo:

 • Vigezo vyote vya kustahihiki kama ilivyoainishwa katika sehemu ya “kiasi cha ruzuku na ustahiki” vinavyotimizwa.
 • Uadilifu wa uhariri wa shirika, uwezekano wa kutoa uandishi wa habari unaozingatia maslahi ya umma na na ufafanuzi wetu wa Vyombo vya Habari vyenye Maslahi ya Umma.
 • Historia, umahiri, na utofauti wa shirika na timu.
 • Athari za ufadhili zinazoweza kutokea – ikijumuisha upatanishi wa maono au shughuli zinazopendekezwa na malengo ya wito huu wa ufadhili na athari inayotarajiwa ya ufadhili kulingana na ufafanuzi wa mwombaji wa jinsi mafanikio yatakavyokuwa.

Katika hatua ya pili, mapendekezo ya waombaji waliochaguliwa yatatathminiwa kwa kuzingatia uwezo wa athari, ubora wa mpango wa kufikia malengo yaliyopendekezwa, mahitaji ya kifedha ya mwombaji na uwiano kati ya ufadhili ulioombwa na malengo yaliyopendekezwa, uwezo na kujitolea kwa timu katika kuzingatia uthabiti na maendeleo ya shirika na kujitolea katika kujifunza. Maelezo zaidi yatatolewa kwa waombaji waliochaguliwa pamoja na fomu ya kuwasilisha mapendekezo.

Jinsi ya kutuma maombi

Kamilisha orodha yetu ya mahitaji na fomu ya dokezo la dhana ili kuomba.

The International Fund for Public Interest Media is an independent fund made possible by the generous financial support of: