Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Malengo ya ufadhili

Changamoto yetu inahusu sana kuhakikisha kwamba tunaweza kuendelea kufadhili utoaji ripoti wetu kutokana na shinikizo la kifedha tunalokabiliana nalo, kuliko kuendeleza shughuli mpya. Je, tunaweza kuomba ufadhili ili tuendelee na shughuli zetu za sasa?

Ndiyo. Utastahli kutuma ombi ikiwa ombi lako la ufadhili ni kusaidia shughuli zilizopo (ikiwa shughuli hizi zitalingana na malengo ya wito huu kwa watu wote).


Je, maombi yetu yatahitaji kuhusisha shughuli zote zilizoainishwa katika wito wa mapendekezo?

Hapana. Si lazima uzungumzie mifano yote iliyoelezwa katika malengo ya ufadhili huu.


Tunatoa huduma (au maudhui, au huduma za kukagua ukweli, au masuluhisho ya teknolojia) kwa mashirika ya vyombo vya habari, lakini hatusambazi habari kwa umma. Je, bado tunaweza kuomba ufadhili katika awamu hii?

Hapana. Katika wito huu wa ufadhili waombaji wanaoruhusiwa ni mashirika ya vyombo vya habari yanayosambaza habari kwa umma. Wito wa ufadhili wa siku zijazo unaweza kujumuisha mashirika yanayotoa huduma kwa mashirika ya vyombo vya habari.

Upeo wa kijiografia

Je, maombi ya ruzuku yanaweza kuhusisha zaidi ya nchi moja?

Hatutarajii maombi ya ruzuku yahusishe zaidi ya nchi moja, lakini yakihusisha zaidi ya nchi moja lazima nchi zote ziwe ndani ya upeo wa kijiografia.


Je, ruzuku zitatolewa katika nchi zote zilizoorodheshwa katika upeo wa Kijiografia?

Si lazima. Kuna kiasi kidogo cha ufadhili kinachopatikana katika wito huu wa kwanza. Tunatarajia kwamba ruzuku iliyowekwa itajumuisha nchi zote zilizoorodheshwa katika upeo wa kijiografia, lakini huenda kuna baadhi ya nchi ambazo hazijachaguliwa kupata ruzuku yoyote katika wito huu wa kwanza.


Je, ruzuku zinapatikana kwa vyombo vya habari vilivyopigwa marufuku/vya nchi za ugenini zilizoorodheshwa katika upeo wa kijiografia?

Inategemea. Ruzuku hazipatikani kwa watu binafsi, zinapatikana tu kwa mashirika ya vyombo vya habari. Ikiwa shirika la kisheria linaloomba ufadhili limesajiliwa katika nchi tofauti na nchi ambayo maslahi ya umma yanazingatiwa katika utangazaji, ruzuku zinaweza kupatikana. Jambo hili litatathminiwa kulingana na hali.

Kiasi cha ruzuku na ustahiki

Je, kuna kiasi kidogo sana cha ruzuku?

Hapana. Hakuna kiasi kidogo sana cha ruzuku iliyobainishwa katika wito huu wa ufadhili lakini kuna sharti kwamba waombaji wawe na mapato ya kila mwaka ya $50,000. Tunatarajia kwamba waombaji wengi watakuwa na mapato ya kila mwaka yanayozidi $50,000.


Maagizo yanabainisha kwamba ruzuku kwa mwaka inatarajiwa kuwa kati ya 10% -30% ya bajeti ya sasa ya mwaka. Ikiwa maombi yetu ya ruzuku ni chini ya 10% au zaidi ya 30% ya bajeti yetu ya sasa, je, hii itachukuliwa kuwa inastahiki?

Ndiyo. Kiwango hiki kinaashiria. Tutazingatia maombi ya asilimia ya chini na ya juu. Kwa asilimia ya ruzuku zaidi ya 30% waombaji watatarajiwa waeleze jinsi wanavyokusudia kupunguza hatari ya kutegemea mfadhili mmoja.


Shirika letu linazingatia utangazaji wa maslahi ya umma kama sehemu ya seti pana ya huduma. Je, bado tunaweza kuomba ufadhili?

Ndiyo. Lakini lazima ruzuku itumike kusaidia uzalishaji wa ripoti za maslahi ya umma na sio kufadhili shughuli nyingine.


Tafadhali unaweza kutoa mfano wa uhusiano unaotarajiwa kati ya kiasi cha ruzuku na bajeti ya sasa. 

Hatua ya 1 ni kuhesabu kiasi cha ruzuku unachoomba kwa mwaka. Kwa hivyo ikiwa ruzuku yako ni ya zaidi ya miaka 2 unapaswa kugawanya kiasi chako cha ruzuku mara mbili. Hatua ya 2 ni kulinganisha kiasi hiki cha ruzuku cha kila mwaka cha wastani na bajeti yako ya sasa.

Matarajio ni kwamba ombi lako la kila mwaka la ruzuku litakuwa kati ya 10% -30% ya bajeti yako ya sasa.

Mfano mzuri:

Ombi la ruzuku: $150,000

Kipindi cha ruzuku: Miaka 2

Bajeti ya sasa: $300,000

Hatua ya 1: Hesabu ruzuku ya kila mwaka ya wastani

$150,000/miaka 2 = $75,000 kwa mwaka

Hatua ya 2: Linganisha na bajeti ya sasa

$75,000 ruzuku ya kila mwaka/$300,000 bajeti ya sasa = 25%

Hii inalingana na kiwango kinachotarajiwa (10%-30%).


Are national funds eligible for IFPIM funding?

Not through this initial call, but yes, we would love to hear from you to explore future IFPIM funding for national funds.

Mchakato wa kutuma maombi na uteuzi

Je, ninaweza kujadili muhtasari wangu wa mradi na mwanatimu wa IFPIM?

Sio katika hatua hii. Ikiwa swali lako halijajibiwa hapa tafadhali tuma swali lako kabla ya tarehe 20 Mei kwenye: opencall@ifpim.org na uandike mada ya barua pepe yako hivi ‘Swali linalohusiana na Wito wa 1 wa Ufadhili’. Tafadhali jua kwamba hatutajibu barua pepe mahususi lakini tutasasisha ‘maswali yanayoulizwa mara kwa mara’ wakati wa mchakato wa kutuma maombi.


Je, ninahitaji kuwasilisha muhtasari wangu wa mradi katika lugha gani?

Ikiwa unaweza kuwasilisha muhtasari wako wa mradi kwa Kiingereza, tafadhali fanya hivyo. Vinginevyo unaweza kuwasilisha katika lugha yoyote ambayo fomu ya muhtasari wa mradi imetafsiriwa.


Je, nani hufanya maamuzi kuhusu mashirika yanayofadhiliwa? Je, wafadhili wenu wanashawishi vipi maamuzi haya?

IFPIM ni mfuko unaojitegemea. Maamuzi ya ufadhili yatafanywa na timu ya usimamizi ya IFPIM. Wafadhili hawawezi kushawishi maamuzi ya ufadhili.


Je, fedha hizo zitatolewa lini? Je, nijumuishe ruzuku katika bajeti yangu ya mwaka ujao au mwaka huu?

Ufadhili utatolewa muda mfupi baada ya mikataba ya ruzuku kusainiwa, lakini hii inaweza kutegemea mamlaka.


Ikiwa shirika letu halijachaguliwa katika wito huu wa kwanza wa ufadhili, je, tunaweza kutuma maombi tena katika wito wa ufadhili za siku zijazo?

Ndiyo. Iwe unaomba ufadhili katika wito huu wa kwanza au ikiwa hauombi ufadhili, utaweza kutuma maombi katika wito wa siku zijazo, mradi unatimiza vigezo vya wito huo.


Je, ruzuku ya IFPIM kwa shirika langu itawekwa wazi?

Kama kanuni ya jumla tutachapisha orodha yetu ya wafadhiliwa. Iwapo jambo hili litasababisha hatari (ya usalama, ya kisiasa…) kwa shirika lako, tutajadiliana nawe na tunaweza kuamua kutotoa taarifa ya ruzuku kwa umma


Je, iwapo shirika langu haliwezi kutuma maombi kabla ya tarehe ya mwisho ya wito huu?   

Huu ni wito kwanza tu wa IFPIM na nyingi zitafuata. Ikiwa ungependa kutuma maombi katika siku zijazo, tutumie maelezo yako kwenye opencall@ifpim.org.

The International Fund for Public Interest Media is an independent fund made possible by the generous financial support of: